
Jaji Lubuva amesema mgombea huyo amewazidi wagombea wenzake kwa kupata kura milioni 8,882,935, hivyo kuwa na asilimia 58.49 ya kura zote.
"Dr. Magufuli(CCM) amepata kura 8,882,935 sawa na 58.46%, Lowassa(CHADEMA) kura 6,072,848, Kwakuwa Dr. Magufuli amepata kura kuliko mwingine yeyote; Tunatangaza rasmi kuwa Amechaguliwa kuwa Rais wa Tanzania", alisema Jaji Lubuva.
Jaji Lubuva amesema shughuli za kumkabidhi cheti cha ushindi Dr. Magufuli zitafanyika kesho kwenye viwanja vya Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam.
Dr. John Magufuli atakuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu kujipatia uhuru wake mwaka 1961, sambamba na mgombea mwenza wake Bi. Samia suluhu, ambaye anatarajiwa kuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa ni mwanamke wa kwanza Tanzania Kushika wadhifa huo.