Baadhi ya watu wenye ulemavu wakiwa wamekaa katikati ya barabara za Uhuru na Kawawa na kusababisha adha ya usafiri katikati ya jiji.
Hatua ya walemavu hao kufunga barabara ni sehemu ya kuushinikiza uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kutimiza ahadi ya kuwaruhusu kurudi na kufanya biashara katika maeneo waliyoondolewa wakati wa zoezi la kuwaondoa watu wanaofanya biashara kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
Katika mahojiano na EATV, walemavu hao wamelalamikia kitendo cha kuondolewa katika maeneo waliyokuwa wanafanya biashara za kuwaingizia kipato, hatua waliyodai kuwa imesababisha maisha yao kuwa magumu.