Sunday , 29th May , 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema serikali iko mbioni kujenga barabara za juu (fly-over) saba mojawapo ikitarajiwa kujengwa Mwenge, ili kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.

Kuongezeka kwa barabara hizo kutalifanya jiji la Dar kuwa na jumla ya fly-ova tisa, baada ya ujenzi wa nyingine mbili kufanyika katika makutano ya barabara ya Ubungo na Tazara.