Monday , 23rd May , 2016

Wafanyabiashara wa dagaa katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam wamesema kuwa kumekuwa na upungufu mkubwa wa dagaa wanaotoka Mkoa wa Kigoma kwa hivi sasa na hata dagaa wachache wanaopatikana wanauzwa kwa bei ghali.

Wafanyabiashara wa dagaa katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam wamesema kuwa kumekuwa na upungufu mkubwa wa dagaa wanaotoka Mkoa wa Kigoma kwa hivi sasa na hata dagaa wachache wanaopatikana wanauzwa kwa bei ghali zaidi hali inayochangiwa na uwepo wa walanguzi wa dagaa ktoka nje ya nchi.

Wakiongea na East Africa Radio wafanyabiashara hao wamesema kuwa hapo awali bei ya kilo ya dagaa wa Kigoma ilikuwa shilingi 18,000 lakini kwa hivi sasa dagaa hao wanapatikan kwa bei ya shilingi 25,000 kwa kilo na wengi wanapelekwa nje huku wanaouzwa nchini wakiwa ni wachache.

Wakati hayo yakiendelea upande wa dagaa wa Kigoma, hali ni tofauti kwa dagaa wanaotoka Mwanza kwani dagaa hao wameshuka bei kutoka shilingi 7,00 kwa kilo hadi kufikia shilingi 4,000 kwa kilo huku upatikanaji wake ukiwa ni wa kuridhisha.