Wednesday , 19th Nov , 2014

Chama cha Wananchi CUF kimesema kitasusia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwaka huu kama serikali (TAMISEMI) haitabadilisha kanuni za uchaguzi huo ambazo anadai kuwa zina lengo la kuvikandamiza vyama vya upinzani.

Naibu Katibu Mkuu CUF (Bara)

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CUF Tanzania bara Magdalena Sakaya amesema serikali ya Tanzania imekurupuka kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu kwani haikuwa na mpango kamili kuendesha uchaguzi huo.

Sakaya amesema viongozi wa serikali wamekuwa wakitoa taarifa zinazokinzana juu ya uchaguzi huo kati ya Rais na Waziri Mkuu, ambapo Rais alisema katika kikao cha mashauriano ya vyama vya siasa kilichoandaliwa na TCD kuwa uchaguzi huo ungefanyika mwezi Februari mwakani na Waziri Mkuu kutangaza kuwa uchaguzi huo utafanyika
Desemba 14.

Kwa upande wa kiongozi wa CHADEMA bwana Fulgency Mapunda ambaye ni Afisa uhamasishaji Chadema amewataka viongozi wa halimashaurui zote kuacha kuwakandamiza wagombea wa upinzani kwa mashinikizo ya viongozi wa kisiasa.

Naye Diwani wa Kigogo kupitia CCM Richard Chegula amewataka viongozi wa upinzani wkuacha lawama kabla ya uchaguzi kwani waamuzi ni wapiga kura wenyewe.
Kwa upande wa Tamisemi kupitia Mkurugenzi wake wa serikali za mitaa bwana Calist Luanda amefafanua juu ya swala zima la uchaguzi huo, na kusema kuwa tuhuma zinazotolewa siyo za kweli