
Freeman Mbowe pamoja na Mbunge Ester Matiko.
Mbali na viongozi hao wakubwa pia mahakamani hapo ilishuhudiwa mamia ya wafuasi wa CHADEMA waliojitokeza kwaajili ya kusikiliza hatma ya kiongozi wao Freeman Mbowe.
“Tunawaambia wanachama wote kesho saa mbili waje mahakamani, chama chote kitahamia hapa, naomba wanachadema tushikamane kwa ajili ya mwenyekiti wetu.” Amesema Borniface Jacob
Akizungumza nje ya viunga vya mahakama Naibu Katibu Mkuu CUF bara Joel Luhabrua amesema “kwa hali ilivyosasa kuna nguvu ya kutaka kuumiza upinzani, tumeona tuongeze nguvu yetu kwa pamoja, ” Joel Luhabura
Mbowe na Matiko wamerudishwa rumande kwaajili ya kusubiri kusikilizwa kwa kesi ya kupewa au kutopewa dhamana, Alhamisi ya wiki hii saa mbili asubuhi.