Thursday , 17th Nov , 2016

Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) limesisitiza haja ya Tanzania kuwa na viwanda vyake vya kuchenjua na kuongezea thamani bidhaa za madini na kuacha kusafirisha nje madini ghafi kwani uwezo wa kufanya hivyo upo.

Samuel Nyantahe

Mwenyekiti wa CTI Bw. Samuel Nyantahe, amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam, wakati wa kongamano la uwekezaji ambalo limejikita katika kuangalia namna ya kuongeza uwekezaji kwenye viwanda vya kuongeza thamani ya madini na vito.

Hoja ya Bw. Nyantahe imeungwa mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF, Godfrey Simbeye ambaye amewataka wafanyabiashara kujiamini na kwamba yeyote atakayeona ananyanyaswa asisite kuwasiliana na TPSF ili nayo iwasilishe malalamiko husika serikalini.

Katika kongamano hilo, Kituo cha Uwekezaji nchini kimewakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake Bw. Clifford Tandari ambaye amesema kama mlezi wa wawekezaji CTI itahakikisha inajenga mazingira mazuri kwa wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi.