Wajumbe hao ni mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka, mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge na mbunge wa Sengerema Wiliam Ngeleja.
Akitoa taarifa ya Kamati Kuu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Nape Nnauye amesema maamuzi hayo yamefikiwa leo katika kikao cha kamati kuu kilichofanyika kwa siku moja jijini Dar es salaam na kuongozwa na mwenyekiti wake Dkt Jakaya Kikwete.
Amesema kuwa wajumbe hao wa NEC ambao ni wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano hawatakiwa kuhudhuria kikao chochote cha NEC wakati taratibu nyingine zikifuata.
Amesema pia chama kimetoa maagizo kadhaa kwa serikali kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi dhidi ya wote waliohusika katika sakata la Tegeta Escrow.
Kuhusu baadhi ya wanachama walioanza kampeni za urais kabla ya wakati, Nape amesema kuwa uchunguzi zaidi unahitajika kufanyika dhidi yao ili kubaini makosa mahususi, na maamuzi yatatoka wakati wowote.
Wanachama hao ni Wiliam Ngeleja, Stephen Wasira, Edward Lowassa, January Makamba na Fredrick Sumaye.