Friday , 3rd Jun , 2016

Chama cha kutetea abiria nchini Tanzania (CHAKUA) kimeiomba Serikali kutositisha huduma zinazotolewa na magari ya abiria ya kawaida maarufu kama daladala zinazopita maeneo ambayo kuna magari ya mwendo kasi kwani huduma za mabasi hayo yanachangamoto.

Chama cha kutetea abiria nchini Tanzania (CHAKUA) kimeiomba Serikali kutositisha huduma zinazotolewa na magari ya abiria ya kawaida maarufu kama daladala zinazopita maeneo ambayo kuna magari ya mwendo kasi kwani huduma za mabasi ya mwendo kasi zinaonekana kuwa na changamoto nyingi.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam. Mwenyekiti wa CHAKUA Bw Hassan Mchanjama amesema kuwa mengi ya mabasi hayo yanakatisha safari na hayafiki katika baadhi ya maeneo na yanasitisha huduma za usafiri mapema zaidi hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa abiria.

Aidha CHAKUA inaagiza vyombo vya dola vinavyosimamia usalama barabarani kuwachukulia hatua madereva wa mwendo kasi kama wanavyochukua kwa madereva wengine wa daladala pale wanapobainika kuvunja sheria za barabarani ikiwa ni pamoja na kukatiza ruti.