
Dkt. Mashinji amesema wabunge wanaohama na kujiuzulu CHADEMA hawaiyumbishi chama hicho tu bali wanayumbisha wadau wote wa uchaguzi pamoja na wananchi ambao ni walipa kodi, maana mchakato wa uchaguzi unatumia fedha na fedha hizo ni kodi za wananchi.
"Upande wa pili umeamua kujitoa ufahamu unafikiria kwamba kwa kufanya siasa za kuwapa watu rushwa wa upinzani kuhamia kwao kunadhohofisha vyama vya upinzani, na kuwaahidi kuwapa nafasi zile zile walizokuwa nazo upinzani hata kama walishindwa kwenye kura za maoni”, amesema Mashinji.
Katibu huyo ameongeza kuwa tabia hiyo inaonekana wazi mpaka na ushahidi tayari ulishapelekwa kuanzia kwenye lile sakata la madiwani huko Arumeru walinunuliwa na Mh. Lema na Nassari walipeleka ushahidi TAKUKURU, hivyo CHADEMA haina shida nao wanaohama kwa sababu wanatumia haki yao kikatiba", amesema Dkt. Mashinji.
Hivi karibuni upinzani umeondokewa na Mwenyekiti wa baraza la Vijana taifa (BAVICHA), Patrobas Katambi pamoja na Godwin Aloyce Mollel ambaye alikuwa Mbunge wa Siha (CHADEMA).