Sunday , 23rd Nov , 2014

Chama cha mapinduzi CCM kimesema hakita sita kuwachukulia hatua watumishi au viongozi watakao bainika katika sakata la Tegeta Escrow.

Chama Cha Mapinduzi kimetoa tamko juu ya sakata la fedha za akaunti ya Tegeta Escrow na kusema hakitasita kuwachukulia hatua watumishi au viongozi wa serikali, waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi endapo watabainika kukiuka maadili na miiko ya uongozi wa umma .

Akitangaza uamuzi na msimamo huo kwenye mkutano wa hadhara mkoani Lindi, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM taifa, Nape Nnauye, amesema kwa muda wote chama hicho kimekuwa kikiwashughulikia hata kuwavua nyadhifa viongozi wote waliotuhumiwa kwa kukiuka maadili na miiko ya uongozi .

Akihutubia mamia ya wananchi wa mkoa wa Lindi kwenye hitimisho la ziara ya siku Nane mkoani humo, Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa chama hicho kujitathimini kama wanakubalika kuliko kusubiri kuwajibishwa au kutimuliwa kwenye uongozi .