Tuesday , 23rd Jun , 2015

Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika mkoa wa Geita kwa kutumia mfumo mpya wa BVR, linatishia kuvunja ndoa za watu kufuatia baadhi ya wanawake walioolewa kulazimika kuacha miji yao na kukesha vituoni.

Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika mkoa wa Geita kwa kutumia mfumo mpya wa BVR, linatishia kuvunja ndoa za watu kufuatia baadhi ya wanawake walioolewa kulazimika kuacha miji yao na kukesha vituoni.

Akinamama wajawazito, walemavu na wazee vikongwe pia wanalazimika kulala vituoni ili kupata nafasi ya kuandikishwa mapema kutokana na baadhi ya vituo kutokuwa na utaratibu wa kuwapa kipaumbele katika zoezi hilo.

Uchunguzi uliofanywa na EATV katika vituo vya kuandikishia wapiga kura vya 14 Kambarage kata ya Buhalahala pamoja na vituo vingine vya kata za Bombambili, Ihanamilo na kijiji cha Kakonda wilayani Geita umeonesha kuwa zoezi hilo limegubikwa na dosari mbalimbali, ikiwemo uchache wa mashine za BVR kwenye vituo, ubovu wa mashine zenyewe, kasi ndogo ya waandikishaji na misururu mirefu ya watu.

Katika uchunguzi huo EATV pia imezungumza na mmoja wa wazee aliyejitambulisha kwa jina la Thereza Kapiga ambaye amelalamikia utaratibu mbovu wa zoezi hilo ambao unawasababisha kushinda njaa.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa 14 Kambarage katika mamlaka ya mji mdogo wa Geita mfaume Nkerebe akieleza adha wanayoipata kama viongozi katika kuhakikisha akinamama wajawazito wanaandkishwa kabla ya muda uliotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC haujamalizika.