Tuesday , 23rd Feb , 2016

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu amezindua rasmi mfumo wa utoaji elimu kwa watumiaji huduma za kifedha ili kuondoa malalamiko yanayotokana na uelewa mdogo wa huduma hiyo.

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu

Prof. Ndulu ameutaja mfumo huo uliobuniwa na mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha Tanzania (FSDT), kama hatua ya kimapinduzi kuwasaidia\wateja wote wa hudumza za kifedha kujua haki na wajibu wao.

Profesa Ndulu amesema wateja wengi wakishakosea katika utumaji wa pesa wanashindwa kuelewa ni mahali gani wanaweza kupata haki zao za kurejesha fedha ambayo imepotea wakati akifanya muamala wa kifedha.

Hadi kufikia mwaka 2014 ni asilimia 57 tu ya watu wazima walitumia huduma za kifedha lakini kwa kiwango cha chini na kuongeza kuwa mfumo huo unatarajiwa kuingizwa rasmi katika elimu ya msingi na sekondari na kuzihusisha taasisi zote za kifedha nchini.

Mratibu wa mpango huo amesema kuwa watu wengi wanahitaji kukopa lakini kinachowashinda ni namna ya kukokotoa riba pamoja na kuogopa kujihusisha na mikopo kutoka katika taasisi za kifedha.