Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu.
Hayo yalisemwa jana na Mchumi kutoka BOT kanda ya kati Dk, Zegezege Mpemba wakati akizungumza na East Africa Radio kwenye banda lao la maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayoendelea katika viwanja vya nanenane vilivyoko mjini hapa.
Dk, Mpemba amesema kuwa wakazi wengi wa mikoa ya kanda ya kati inayosimamiwa na BOT inakabiliwa na tatizo la noti chakavu ambazo hawajuwi mahali pa kuzipeleka na kuwataka kuziwasilisha katika banda hilo Agosti 6 mwaka huu ili ziweze kubadilishwa.
Kwa upande wake Dominic Mwita ambaye pia ni mchumi wa BOT amewataka wananchi kufika kwenye maonyesho hayo ili waweze kujua ni namna gani