Wednesday , 2nd Apr , 2014

Baadhi ya wafanyabiasha katika eneo la kariakoo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, wamelalamikia hatua ya uongozi wa manispaa ya Ilala ya kuendesha zoezi la kuvunja sehemu zao za biashara pasipo taarifa na wala wenyewe kuwepo wakati wa zoezi hilo.

Wakizungumza na East Africa Radio, baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema kitendo cha maduka yao kuvunjwa usiku wa manane pasipo wao kuwepo kinaweza kutafsiriwa kuwa ni wizi kwani hakiendani kabisa na utaratibu wa utawala wa sheria.

Mmoja wa wafanyabiashara hao ni aliyefahamika kwa jina moja la Bw Mchapakazi ambaye anaituhumu manispaa hiyo kuvunja duka lake lililopo katika makutano ya mitaa ya Mchikichi na Sikukuu eneo la kariakoo usiku wa kuamkia leo na kumsababishia hasara kubwa.