Friday , 25th Mar , 2016

Hatua ya Uganda kufikia makubaliano na nchi ya Tanzania kujenga bomba la kusafirishia mafuta kutoka Ziwa Albert nchini Uganda mpaka bandari ya Tanga nchini Tanzania linaonekana kuzua mvutano wa kidiplomasia na nchi ya Kenya.

Picha za Marais wa Nchi ya Tanzania, Uganda na Kenya ambao wanavutana kuhusu Ujenzi wa bomba la mafuta

Hivi karibu Maafisa kaadha wa nchini Kenya akiwemo Waziri wa Nishati Charles Keter, walizuiliwa kuingia katika bandari ya Tanga ambako ujumbe wa Uganda ulitembelea katika bandari hiyo ili kukagua miundo mbinu ya ujenzi wa Bomba hilo.

Duru za Habari kutoka nchini Kenya zimetaarifu kuwa maafisa wa Kenya walifika bila mwaliko wa mwenyeji wao ingawa waliambatana na Ujumbe kutoka Uganda ambao uliwahi kufanya ziara katika Bandari ya Lamu na Mombasa siku za hivi Karibuni

Hapo awali Serikali ya Kenya iliweza kuishawishi Uganda Kujenga bomba hilo kupitia nchini mwao ambapo baada ya rais wa Uganda Yoweri Museveni kukutana na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ndipo Serikali ya Uganda ilipobadili maauzi ya Ujenzi wa Bomba hilo.

Baada ya Ugunduzi wa Mafuta kuzunguka Ziwa Albert, Uganda sasa inataka kusafirisha Mafuta Nje lakini bado kumejitokeza sintofahamu ya Bandari ipi ambayo itasafirisha mafuta hayo kwenda nje ya nchi.