Mweyekiti wa bodi yaTumbaku nchini Said Nkumba akizungumza na Waandishi wa Habari.
Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa tumbaku kutoka mikoa yote inayolima zao hilo,Mweyekiti wa bodi ya hiyo nchini Said Nkumba amesema imekuwepo tabia kwa vyama vya wakulima binafsi kuchukua mikopo kwa kutumia mgongo wa wakulima walioko kwenye vyama vya ushirika na baadaye kukiuka makubaliano kwa kuuza tumbaku kwa kutumia vyama vyao huku wakiwaacha wakulima wengine wakilipa madeni yaliyoachwa na wengine.
Kwa upande wa wadau wa tumbaku akiwemo Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya ameitaka serikali kuwapa kipaumbele wakulima wa zao hilo na kutambua mchango wake katika kuiliingizia taifa fedha za kigeni tofauti na mazao mengine sambamba na kuangalia mfumo wa bei elekezi itakayokuwa na tija kwa wakulima.
Mkutano wa wadau wa zao la tumbaku umefanyika mkoani morogoro kwa kuwashirikisha wadau wa zao hilo na umejadili changamoto na mafanikio yaliyopo katika uzalishaji wa zao hilo.