Thursday , 8th Dec , 2016

Ikiwa ni siku chache baada ya kiwanda cha Dangote Industries Limited cha Mtwara kusitisha uzalishaji wa Saruji, wananchi wilayani Tandahimba wamelalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo jambo ambalo linapelekea kukwamisha shughuli za ujenzi.

Mifuko ya saruji

 

Wakizungumza wilayani humo baada ya kumalizika kwa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani, wananchi hao wamesema kuwa bidhaa hiyo imepanda ghafla kutoka bei ya shilingi 11,500 mpaka 17,500 katika kipindi cha wiki moja.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akifunga mafunzo hayo, akawataka baadhi ya wananchi kuacha tabia ya kuweka matuta holela barabarani ambayo yanaweza kusababisha ajali kwa waendesha bodaboda na watumiaji wengine.

Wasikilize hapa  Osman Gaswa na Rashid Chande wakazi wa Tandahimba pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo.

Wananchi Osman Gaswa na Rashid Chande
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba - Sebastian Waryuba