Friday , 20th May , 2016

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema fedha nyingi zinazopelekwa kwenye serikali za mitaa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hazionyeshi thamani ya fedha.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa.

Profesa Mbarawa amesema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi ya makao makuu ya bodi ya mfuko wa barabara mjini Dodoma, na kusema kuwa kupitia ziara aliyofanya katika baadhi ya mikoa ameziona barabara zilizo chini ya kiwango.

Mhe. Mbarawa amesema kuwa ujenzi wa barabara sekta Muhimu ambayo inahitaji fedha nyingi ambapo amesema bado kuna changamoto ya matumizi ya fedha hizo katika utengenezaji wa miundombinu hiyo.

Aidha, Waziri Mbarawa amesema kuwa miundombinu ya barabara, reli, pamoja na bandari ina umuhimu wa kipekee katika ukuaji wa sekta ya viwanda ambayo ndio dira ya taifa kufikia mwaka 2025.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt. James Wanyacha, amesema kuwa kulingana na hali ya barabara nchini amesema kiasi cha fedha kinachopatikana bado hakikidhi matengenezo ya miundombinu hiyo.