Thursday , 8th May , 2014

Kaimu mkuu wa mkoa wa Lindi nchini Tanzania Agnes Hokororo ameisitisha kwa muda safari za Dar kwenda Lindi hadi Mtwara kufuatia kuharibika kwa barabara katika eneo la Marendego Pwani.

Baadhi ya mabasi ya abiria yanayofanya safari zake kati ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara, yakiwa yamekwama eneo la Nyamwage mkoa wa Pwani kutokana na ubovu wa barabara.

Akizungumza kwa njia ya simu na East Africa Radio, Bi. Hokororo amesema wamelazimika kuchukua uamuzi huo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kuharibu vibaya eneo hilo.

Amewashauri wananchi ambao watakuwa hawana ulazima wa kusafiri kuacha kusafiri wakati huu ambapo serikali inajaribu kuangalia namna ya kukarabati eneo hilo lililoharibika vibaya.