Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bi. Janeth Ruzangi
Akizungumza jana ofisini kwake meneja mawasiliano wa bandari nchini Janeth Ruzangi amesema kuwa wameboresha mfumo wa uingiaji katika bandari hiyo kwa wahusika na wageni ili kuepusha wizi usio walazima.
Ruzangi amesema kuwa wameanza kufunga CCTV Camera ndani ya bandari yote pamoja na kuwa na chumba maalum cha uangalizi wa camera hizo lakini pia mradi huo umeanzia bandari ya Dar es salaam lakini wataweza kuufanya kwa bandari zote nchini.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha usalama bandari Lazaro Twanga amewahakikishia wateja wanaotumia bandari hiyo kutokana na mfumo waliouweka, hakutakuwa na upotevu wa mizigo yao tena.
Bw. Lazaro amesema kuwa mradi huo utakuwa na jumla ya camera 486 ambazo zitazunguka maeneo yote ya bandarini ikiwemo maeneo ya huduma za mafuta pamoja na maeneo ambayo meli ambazo haziwezi kuingia baharini zinakuwepo.
Zaidi ya shilingi bilioni tisa zinatarajiwa kutumika katika kuhakikisha ulinzi pamoja na vitengo vyote muhimu lengo likiwa ni kudhibiti mianya ya upotevu iliyokuwa inatumiwa na viongozi wasiokuwa waadilifu.