Thursday , 14th Jan , 2016

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa amesema ili kukabiliana na ufujaji wa mapato katika vivuko vya Kigamboni serikali itaanzisha mfumo mpya ya uvushaji wa magari pamoja na ulipaji tiketi.

Mhandisi Karim Mattaka (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto)

Prof Mbarawa amesema hayo jana wakati alipofanya ziara katika kivuko cha Kigamboni/Magogoni jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa mfumo huo utawezesha abiria waweze kulipia huduma hiyo kwa mwaka kwa wale wenye uwezo huo.

Aidha Pro. Makame amekiri kuwepo kwa mapungufu katika vivuko hivyo ikiwemo eneo dogo la kusubiria abiria pamoja na miundo mbinu ya walemavu hivyo kuwataka TEMESA kuboresha hali hiyo.

Aidha waziri Mbarawa ameongeza kuwa katika kuendelea uboreshaji wa vivuko hivyo serikali imepanga katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha kununua kivuko kingine na kufanya vivuko kuwa vitatu ili kukidhi mahitaji ya wananchi wanaotumia usafiri huo.