Wednesday , 12th Aug , 2015

Serikali imesema licha ya kuendelea na Uchunguzi wa kubaini ugonjwa uliomuua Mkimbizi mmoja katika kambi ya Nyarugusu ambae inasadikiwa amefariki kwa ugonjwa wa ebola imewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa huo.

Mtaalam wa ufuatiliaji wa magonjwa ya binadamu wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Vida Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu historia ya ugonjwa wa Ebola.

Mtaalamu wa Ufatiliaji na Udhibiti wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania Dkt. Vida Mmbaga amesema kuwa mgonjwa huo amefariki dunia akiwa na dalili kadhaa za Ugonjwa wa ebola lakini bado wanaendelea kufanya uchunguzi kwa kuwa kuna dalili nyingine hakuwa nazo.

Dkt. Mbaga amesema serikali inaendelea kuchukua hatua za kuchunguza watu wote wanaotokea nchi za Afrika Magharibi kwa kuwa ugonjwa huo bado upo lakini amewatoa hofu Wananchi kuhusu ugonjwa huo kuingia nchini.

Dkt. Mbaga ameogeza kuwa Mgonjwa huyo alikua chini ya Uangalizi maalumu ambapo alitakiwa kusafirshwa kuelekea nchini Marekani lakini bahati mbaya amefariki kabla ya kupelekwa huko.

Ameongeza kwa vipimo vimeshachukulia na kupelekewa katika hosptali ya Muhimbili kwa ajili ya uchugnuzi Zaidi na baadae Serikali itatoa majibu sahihi juu ya Ugonjwa ulipelekea kifo cha Mgonjwa huyo kama ni ebola au la.