Mkurugenzi wa Watetezi wa Haki za Binadamu Onesmo Ole Ngurumwa,
Akiongea kwa niaba ya AZAKI, mratibu wa muungano wa asasi za kiraia za kutetea haki za binadamu THRDC Onesmo Olengulumwa amesema kuwa katika Ilani yao yapo maeneo yakifanyiwa kazi vizuri basi maisha ya watanzania yatabadilika tofauti na sasa ambapo kuna upungufu wa huduma muhimu hasa katika sekta za afya, maji, elimu na huduma za kijamii.
Olengulumwa ameongeza kuwa taifa linahitaji sera ya pamoja ya uchumi ili kuinua uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na usimamizi mzuri wa rasilimali za nchi ili ziwanufaishe wananchi wote.
Aidha asasi hizo za kiraia zimemtaka rais mteule Dr. Magufuli ashughulikie masuala ya haki za binadamu pamoja na kubadili mfumo uliopo ambao utatoa fursa ya kuwa na tume huru za uchaguzi na kuimarisha utawala bora.