Tuesday , 14th Jul , 2015

Mtu aliyefahamika kwa jina la Selemani Maporomoko ameuawa kinyama na jirani yake aliyefahamika kwa jina la Mohamed Wajisiku baada ya kuwa na mgogoro wa muda mrefu wa kugombea eneo la shamba lenye heka moj na nusu katika kijiji cha malanje, Mtwara

Kamanda jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Henry Mwaibambe

Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wakazi wa kijiji hicho walioshuhudia wamesema marehemu alikuwa akisafirisha mbao kuelekea mjini kwa kutumia usafiri wa baiskeli majira ya alfajiri, ndipo alipokutwa na shambulio hilo lililotekelezwa kwa kutumia mapanga.

Akithibitisha tukio hilo kwa njia ya simu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara Henry Mwaibanbe amesema marehemu alikutwa na tukio hilo wakati akisafrisha biashara yake ya mbao kwenda mjini kwa baiskeli na ndipo alipoviziwa na jirani yake na kumshambulia kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na hatimaye kupoteza maisha.

Aidha, amesema mtuhumiwa ametoroka, na baiskeli yake ilikutwa eneo la tukio hali iliyowapandisha hasira wananchi na kuamua kwenda nyumbani kwake kuvunja nyumba kubeba kila kitu na hatimaye kuichoma moto nyumba.