Thursday , 21st Jan , 2016

Mwanamke mmoja mkoani Morogoro na mwanaye wa kike wameuawa kikatili nyumbani kwao baada ya baba wa familia hiyo kuwashambulia kwa kitu chenye ncha kali.

Baba wa familia aliyefanya mauaji, akiwa hospitali

Matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yameendelea kujitokeza mkoani Morogoro baada ya mwanamke Elizabet Omari (46) na mwanaye Aisha Abedi (18) wameuawa kikatili nyumbani kwao Mvomero na baba wa familia hiyo na kisha kunywa sumu kwa lengo la kujiua mwenyewe kufuatia ugomvi wa kifamilia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro SACP Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mvomero mkoani Morogoro.

Amesema mwanaume huyo aliwashambulia mkewe na mtoto sehemu za kichwani kwa kitu chenye ncha kali na baadaye mkewe kumchoma na kisu sehemu ya chini ya ziwa la kushoto na mtoto kuchomwa shingoni na kupelekea vifo vyao na baadaye kunywa maji ya betri kwa nia ya kutaka kujiuwa.

Kwa upande wao mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanaume huto ni mfanyabiashara ya madini na kwamba majira ya usiku walisikia mwanamke akipiga kelele ya kuomba msaada.

Naye muuguzi wa zamu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro wodi namba tisa Bi Happyness Lyanga amesema walimpokea Bw Togorani majira ya saa mbili asubuhi na kwamba inaelezwa kuwa mwanaume huyo aliwaua mkewe na mtoto kisha kunywa maji ya betri kwa nia ya kujaribu kujiua lakini kameshindikana na baada ya kutekeleza mauaji hayo alishambuliwa na wananchi wenye hasira.

Nyumba palimotokea mauaji hayo