Sunday , 18th May , 2014

Askofu mstaafu wa kanisa la kiinjili la kilutheri nchini Tanzania, Elinaza Sendoro, amewaonya wafuasi wa UKAWA katika Bunge Maalumu la Katiba kuacha misimamo inayotishia kukwamisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Elinaza Sendoro.

Aidha, askofu Sendoro amewasihi wafuasi hao wa UKAWA kurudi bungeni badala ya kuzunguka nchi nzima kuhimiza wananchi wakubali mapendekezo na misimamo yao dhidi ya ile ya chama tawala CCM.

Katika maelezo yake kwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba, Askofu Sendoro pia amewataka wajumbe kutoka CCM kufahamu kuwa hawana uhalali wa kutamka kuwa katiba mpya ni lazima ipatikane na kwamba kauli hiyo inapaswa kutolewa na Watanzania kupitia kura ya maoni.