Kaimu mkuu wa mkoa wa Njombe na wilaya ya Ludewa, Anatory Choya,
Akizungumza na East Africa Radio, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Njombe na wilaya ya Ludewa, Anatory Choya, amesema kuwa wananchi wa Njombe wamekuwa wakiongoza wa uzalishaji lakini watoto wao wanaongoza kwa kuwa na udumavu pamoja na utapiamlo.
Choya amesema kuwa kunatatizo kubwa katika mkoa huo ambapo amesema wameandaa utaratibu wa kuhakikisha kuwa hali ya udumavu na utapiamlo inaondolewa mkoani humo.
Bw. Choya ameongeza kuwa wakazi hao wamekuwa wakila vyakula dhaifu huku vyakula vizuri na vyenye ubora vikipelekwa sokoni akitolea mfano kwa wakulima wa nyanya ambao huuza nyanya nzuri zote na kubakiwa na zilizoharibika.