
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ibanda Rogers Chebene amesema kuwa mmoja wa watuhumiwa ambaye alishiriki katika zoezi hilo aliamua kutoa taarifa Polisi baada ya kukosa mgao wake wa fedha kama walivyokubaliana.
Watuhumiwa wengine walioshiriki katika tukio hilo wametajwa kuwa ni Keresensio Mwesigye Alias Kamwesi, Experito Kacunguza, Stephen Mukama pamoja na Medrine Kabasiita ambao wote kwa sasa wametiwa nguvuni na jeshi la Polisi.
Aidha mwili wa Marehemu umechukuliwa na kupelekwa katika kituo cha Afya cha Ruhoko kwa uchunguzi zaidi.