Sunday , 24th May , 2015

Baba mdogo wa marehemu anayedaiwa kuuwawa kwa kupigwa na risasi na askari Polisi amesema chanzo cha kifo cha mwanae Basi Mwalongo ni kuwa alikuwa anamdai askari huyo na kuitaka serikali ihakikishe inambana mtuhumiwa ili aeleze chanzo.

Baadhi ya wananchi wakiwa wamefunga barabara baada ya kudai mwenzao mmoja ameuwawa kwa makusudi na Polisi

Amesema kuwa licha ya jeshi la Polisi kumuweka mahabusu mshitakiwa ihakikishe inamuhoji na kuhakikisha haki za marehemu zinapatikana.

Akizungumza baada ya mazishi ya mwanae ambayo yalitakiwa kufanyika Alhamisi ya wiki jana na kushindwa kufanyika siku hiyo kutokana na kibali cha mazishi kuto kuwa na muhuri na kuto eleza sababu ya kifo na kuzikwa Ijumaa.

Baba wa marehemu, Joseph Mwalongo amesema kuwa chanzo cha kifo cha mwanae ambaye alikuwa ni fundi kujenga inadaiwa kuwa alijenga nyumba ya askari anayedaiwa kufanya mauaji na alikuwa anamdai pesa za ujenzi huo wa nyumba.

Amesema kuwa askari huyo alipopata kazi ya kufanya doria usiku inadaiwa alimuona Basil mahari na kuanza kumfuatilia na kisha kumpiga risasi na kusababisha kifo chake.

Licha ya mwili wa marehemu kuzikwa baada ya siku ya kuwaza kukataliwa kuzikwa bado ndugu za marehemu hawakulizika na kibali kilichotolewa mara ya pili baada ya mara ya kwanza kutolewa bila kuandikwa sababu ya kifo.

Wamesema kuwa katika kibali cha pili kilionyesha kuwa marehemu alikufa kwa kuvuja damu nyingi na kufa ambapo kibali hicho kilikuwa kimetolewa na hospitali ya Kibena huku baada ya kuto lizika walimfuata mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba kutoa kibali hicho na mazishi kufanyika.

Katika mazishi hayo upande wa serikali kuliwakilisha na mshauri wa mgambo Reonald Mwajombe kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Njombe amesema kuwa serikali imesikitishwa na msiba huo.

Kwa upande wa jeshi la mpaka siku ya Ijumaa hakukuwa na kauli yoyote huku kamana akisema kuwa anavikao na siku ya Ijumaa Waandishi ilipo fika katika ofisi za kamanda wa polisi alikuwa na kikao na makamanda wa polisi wa wilaya na kuahidi kuzingumza mpaka jioni hakukuwa na chochote alichiozongumza.

Marehemu Basil Mwalongo aliuwawa siku ya Jumanne wiki iliyopita kwa kudaiwa kupigwa na risasi kichwani wiki iliyopita na siku ya jumatano kusababisha maandamano ya wananchi kutoka katika mtaa aliokuwa anaishi wa Nzengelentete ambao walitaka kutoa mwili wa marehemu katika hospitali ya Kibena na kuupeleka katika kituo cha Polisi.

Marehemu alifia katika kilabu ya pombe ya Nyondo katika mtaa wa Kambalage mjini Njombe ambapo siku hiyo Fred Sanga alijeruhiwa ambapo askari hao walikuwa doria na kufanya vurugu kilabuni hapo.