
Picha za ajali.
Kamanda Ng'anzi amesema gari aina ya Land Cruiser iliyokuwa imebeba watalii imegongana uso kwa uso na Lori la mizigo takribani Kilometa 10 kutoka njia panda ya Monduli.
''Nipo eneo la ajali hapa muda huu, tunaendelea na vipimo hapa, nitawajulisha kwa undani lakini vifo vipo ila bado hatujajua ni idadi gani'', amesema.
Baada ya taratibu kukamilika Kamanda Ng'anzi amesema waliofariki ni watano ambao ni watalii wanne kutoka nchi za Hispania na Italia na mwingine aliyefariki ni Mtanzania ambaye alikuwa mpishi wa watalii hao.
Ameongeza kuwa miili imepelekwa katika Hospitali ya Mount Meru huku hali ya dereva wa gari la utalii ikiwa si nzuri.