Tuesday , 14th Apr , 2015

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imekabidhi magari 8 kwa washindi wa mwisho wa shindano la Airtel Yatosha zaidi.

Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya 'Airtel Yatosha Zaidi

Washindi hao waliokabidhiwa magari leo jijin Dar es salaam katika ofisi zao maeneo ya Moroco ni pamoja na Wafanyabiara, mama Lishe, Wanafunzi, Pamoja na kondata wa daladala.

Akiongea wakati wa kukabidhi magari hayo Mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya habari Frank Filmam amewashukuru wateja wa Airtel kwa kutumia huduma za kampuni yao hususani huduma ya Airtel yatosha zaidi ambayo mbali na kuwazawadia wateja wao magari pia imewawezesha kupata unafuu wa mawasiliano kwa kila mtanzania.

Kwa upande wa washindi hao wao wameishukuru kampuni hiyo na kuitaka kuendelea kutoa huduma bora pamoja na promosheni kabambe zenye zawadi kama hii ambayo imeisha rasmi leo.