Friday , 22nd Jan , 2016

Hofu imetanda mjini Dodoma baada ya Ofisa wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoani hapa, Emmanuel Meta (37) kuuawa kwa kushambuliwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia juzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David A. Misime - SACP

Meta alishambuliwa na watu wasiofahamika Januari 20 mwaka huu majira ya saa 6: 15 usiku mtaa wa Area C wakati akitoka Bar ya Rose Garden iliyopo mtaani hapo akirejea nyumbani kwake Mtaa wa Area D ambapo alifariki dunia wakati anapatiwa matibabu.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, David Mnyambuga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi la polisi linamshikilia mtu mmoja kutokanana tukio hilo ambaye hakumtaja jina lake.

Mnyambuga alisema kuwa mtoa taarifa wa awali wa tukio hilo Athumani Mtengwa ambaye pia ni Ofisa ya Takukuru mkoani hapa alisema kuwa marehemu alimpigia simu majira ya saa 6:15 na kumwomba ampeleke hospitali kutibiwa kwa kuwa amepigwa na wezi wakati akirudi nyumbani kwake akitokea bar ya Rose Garden iliyopo Area “C” jirani na nyumbani kwake kwa matembezi.