Friday , 4th Mar , 2016

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Alliance for Democratic change (ADC),Mhe. Hamad Rashid, amethibitisha kuwa chama chake kitashiriki katika uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika tarehe 20 mwezi huu visiwani Zanzibar.

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Alliance for Democratic change (ADC),Mhe. Hamad Rashid,

Akizungumza na wanachama wa chama hicho katika makao makuu ya ofisi hiyo iliyopo mjini Unguja Bububu, Mhe. Hamad amesema kuwa viongozi wa siasa wanapaswa kujua uchaguzi ni haki ya mwananchi wa Zanzibar na kutoka wito kwa vyama vingine kushriki uchaguzi huo wa marudio.

Mhe Hamad amesema kuwa ameshangazwa na baadhi ya vyama vya siasa kugomea uchaguzi huo na kusema kuwa jambo hilo linakwenda kinyume na katiba na kumnyima haki mwananchi kumchagua kiongozi wanayemtaka.

Wakati huo huo Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ally Vuai, amewataka wanawake wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), kuendelea kuwahamasisha kina mama wote visiwani Zanzibar kujitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi wa marudio.

Vuai amesema lengo kuu ni kuweza kukifanya chama hicho kuendelea kuingoza Zanzibari ikiwa ni pamoja na kulinda muungano wa Tanzania pamoja na kuyaenzi na kuyaendeleza Mapinduzi ya Zanzibar