Tuesday , 9th Feb , 2016

Naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Dkt. Khamis Kigwangalla amesema asilimia 15 ya wanawake nchini wamekeketwa ambapo mikoa minne ndiyo kinara wa tatizo hilo.

Dkt. Kigwangalla ametoa takwimu hizo alipokuwa akifunga kongamano la siku ya kupinga vitendo vya ukeketaji na wanawake kwa ujumla.

Ameitaja mikoa ya Manyara, Singida, Mara, Arusha na Dodoma kuwa ndiyo inayoongoza kutokana na imani potofu zilizoenea juu ya wanawake katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa utafiti wa kidemografia na afya Tanzania 2010 unaonyesha kuwa asilimia 15 ya wanawake nchini wamekeketwa huku mkoa wa Manyara ukushika namba moja kwa asilimia 71%

Aidha Dkt. Kigwangala ametoa wito kwa jamii kuepuka vitendo hivyo kwani humharibu mwanamke kisaikolojia, kiafya,kielimu na kimaendeleo.