
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa.
Akithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa, amesema watuhumiwa hao wakiwamo mwanamke ambae ni mganga wa kienyeji katika wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wanashukiliwa na jeshi hilo.
Kamanda Mtafungwa amesema kuwa limeibuka wimbo la wahalfu ambao wanawatumia watoto katika kufanya matukio hayo ili kuwadanganya wana usalama hao wasiweze kufikiria kuwa watoto wanaweza kufanya matukio ya uhalifu.
Kamanda Mtafungwa amesema baadhi ya waliokamatwa ni pamoja na waganga wawili wa kienyeji msichana mwenye umri wa miaka 17 na Mwanamke wa miaka 22 wanaidaiwa kukutwa wakiwapatia huduma mbalimbali watuhumiwa hao.
Katika kipindi cha kisichozidi miezi minne wafanyabishara watano wameuawa kwa kupigwa risasi na kisha wauaji kutokomea pasipo julikana.