Thursday , 13th Dec , 2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ametoa muda wa siku 6 kuanzia leo Desemba 13, 2018 hadi Jumatano ijayo Desemba 19, 2018, kuhakikisha halmashauri ya jiji la Dar es salaam inaanza ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis.

Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo

Jafo amesema ukipita muda huo ujenzi huo haujaanza, basi fedha zilizotengwa kwaajili ya mrafi huo atazihamishia kwenye halmashauri nyingine nchini ili ziweze kutekeleza miradi mingine ya maendeleo.

''Mpaka Jumatano wiki ijayo kama sitopata maelezo ya kutosha ya kuanza kwa ujenzi wa stendi ya mabasi ya jiji la Dar es Salaam, Mbezi Luis, fedha hizo tutazipeleka katika Halmashauri zingine'', amesema Jafo

Aidha Jafo amesisitiza kuwa tayari wameshatuma fedha kiasi cha shilingi bilioni 105 kwenye wilaya 67 kwaajili ya ujenzi wa hospitali za wilaya.

''Pia ifikapo Jumatano wiki ijayo kwa zile wilaya ambayo tumeshatuma fedha na bado hawajaanza ujenzi tutahamishia katika wilaya ambazo zilikuwa kwenye awamu ya pili'', ameongeza.