Submitted by Brendansia on Thursday , 13th Mar , 2014
wasanii waliotembelea mashabiki mbalimbali nchini wakati wa Kili Music Tour 2013 kwenye picha ya pamoja mara Baada ya kuongea na Waandishi wa Habari baada ya Uzinduzi.
Malkia wa miondoko ya dansi maruufu kama Lady Jaydee akitumbuiza mashabiki wake na nyimbo zake kali kwenye Kili Music tour 2013.
Mashabiki wa muziki waliojitokeza mkoani Mwanza kushuhudia shoo ya Kili Music Tour.
Mkali wa miondoko ya slow jam Ben Paul naye akionyesha vitu vyake akiungwa na mwanadada stejini ili kuleta Burudani Zaidi.
Wapenzi wa Hip pop nao walipata burudani safi kutoka kwa mwanamziki Fid q.
Prof. Jay naye akitumbuiza na kuimba na mashabiki wake katika viwanja vya Tanganyika mkoani Kigoma.
Diamond akifanya vitu vyake katika mmoja ya matamasha mikoani.
Lady Jaydee na prof J wakishirikiana Stejini kutoa burudani mwanana kwa washibiki waliofika kushuhudia.
Barnaba na Izzo business wakitoa vionjo mbalimbali kuleta utamu zaidi kwenye shoo.
Snura naye akitoa burudani akicheza wimbo wake maruufu wa "majanga"