Submitted by Telesphory on Thursday , 24th Jul , 2014
Majaji Hassan Nyamwela, Queen Darleen na Lotus Kyamba (mwisho), wakifuatilia kwa makini ubunifu wa kucheza kutoka kwa vikundi vilivyojitokeza kwenye Uzinduzi wa mashindano ya Dance 100% 2014, katika viwanja vya Upanga Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya makundi wakionesha manjonjo yao ya kucheza, katika mashindano ya Dance100% katika uzinduzi wa kwanza uliofanyika kwenye viwanja vya Upanga Don Bosco jijini Dar es Salaam Julai 19 2014.
Baadhi ya mashabiki wakishuhudia michuano ya kuDance kwenye uzinduzi wa mashindano ya Dance100% , katika viwanja vya Upanga Don Bosco jijini Dar es Salaam, Mashindano haya yanadhaminiwa na Vodacom Tanzania na kinywaji rasmi kikiwa Grand Malt.
Majaji Hassan Nyamwela na Queen Darleen wakiwa wamekula pozi kwa ajili ya kupiga picha,
Washereheshaji wa shindano la Dance 100% 2014, Tonny Albert maarufu kama TBWAY 360 na mwenzake Menina Atick (katikati) wakidansi kwa pamoja na makundi yaliyovuka mzunguko wa awali wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Dance 100% 2014,