Submitted by Telesphory on Wednesday , 26th Oct , 2016 Halima ambaye ni mwakilishi wa EATV akikabidhi vitabu kwa mwalimu wa shule ya Brilliant iliyoko Mbezi jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kujenga ushirikiano. Tukio hili liliambatana na tamasha la 5 SELEKT lililofanyika shuleni hapo siku ya Alhamisi ya tarehe 13/10/2016. T Bway ambaye ni Mshehereshaji wa tamasha la 5 Selekt akionyesha ujuzi wake katika kucheza muziki,hii ilikuwa ni katika ufunguzi wa tamasha hili katika shule ya Brilliant iliyopo mbezi, Dar es salaam siku ya alhamisi 13/10/2016. Mshereheshaji wa tamasha la 5 Selekt anayejulikana kwa jina la Vanilla, akiwa jukwaani akiwaonyesha wanafunzi wa shule ya Brilliant iliyopo Mbezi jijini Dar es salaam baadhi ya zawadi zitakazotolewa katika tamasha hilo lililofanyika siku ya alhamisi ya tarehe 13/10/2016. Mshehereshaji wa tamasha la 5 Selekt anayejulikana kwa jina la Vanilla akionyesha kufurahia jambo pamoja na wanafunzi wa shule ya Brilliant iliyopo Mbezi jijini Dar es salaam. Tamasha hilo lilifanyika shuleni hapo siku ya Alhamisi ya tarehe 13/10/2016. Moja ya wanafunzi waliopanda jukwaani kwa ajili ya kuonyesha vipaji vyao katika kucheza muziki katika tamasha la 5 Selekt lililofanyika katika shule ya Brilliant iliyopo Mbezi Dar es salaam siku ya Alhamisi ya tarehe 13/10/2016. Mwanafunzi wa shule ya Brilliant ya Mbezi jijini Dar akiwa anaonyesha kipaji chake cha uimbaji pale alipopanda katika jukwaa la 5 Selekt lililofanyika katika shule hiyo siku ya Alhamisi ya tarehe 13/10/2016. Pembeni ni washehereshaji wa Tamasha hilo hilo T Bway pamoja na Vanilla. Wanafunzi wa shule ya Brilliant ya Mbezi jijini Dar es salaam wakionyesha umahiri wao katika kucheza muziki wa Singeli katika Tamasha la 5 Selekt lililofanyika shuleni hapo siku ya Alhamisi ya tarehe 13/10/2016. Mshehereshaji wa Tamasha la 5 Selekt anayejulikana kwa jina la Vanilla akifurahia jambo pale ambapo baadhi ya wanafunzi walipanda jukwaani kujibu maswali ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali. Tamasha hilo lilifanyika katika shule ya Brilliant ya Mbezi jijini Dar es salaam, likiwa limeandaliwa na kituo cha EATV wakishirikiana pamoja na mtandao wa simu wenye kasi zaidi mtandao wa Vodacom. Msanii wa muziki wa kizazi kipya Young Killer naye alikuwepo katika tamasha la 5 Selekt ili kutoa burudani kwa Wanafunzi wa shule ya Brilliant iliyopo Mbezi. Msanii huyo aliweza kuimba nyimbo zake huku wanafunzi wakionyesha kufurahia burudani hiyo ya muziki kutoka kwa mwanamuziki huyo. Tamasha hilo lilifanyika katika shule hiyo siku ya Alhamisi ya tarehe 13/10/2016.