Mtoto amuwekea sumu mama yake kwenye maharage
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limemkamata John Kandole (11), mwanafunzi wa darasa la 7 katika shule ya Msingi Lwemba kwa tukio la kujaribu kumuua mama yake mzazi aitwaye Regina John Kalinga (44) kwa kuweka sumu kwenye chakula kisa tu anachukizwa na tabia ya mama yake ya kupenda kumtuma.

