Rais Samia atoa pole vifo vya watu 28 Mbeya
Rais Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera kufuatia ajali ya gari iliyotokea Juni 7, 2025, majira ya saa 1 usiku katika eneo la Mlima Iwambi, Tarafa ya Utengule Usongwe, barabara kuu ya Mbeya-Tunduma.