Rais kikwete kutangaza bunge la katiba leo
Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kutaja majina ya wajumbe watakaounda bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza vikao vyake Februari 18 mwaka huu.
Katika orodha ya wajumbe hao Rais Kikwete ametangaza kuwaacha watu 3,553 miongoni mwa waliopendekezwa huku akiwaonya wanasiasa kuweka mbele maslahi ya taifa na kuacha kutumiwa na vyama vyao.