Semina ya Bunge Maalum yahairishwa kwa muda

Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu la Katiba, Pandu Ameir Kificho

Semina ya Bunge Maalum la Katiba imelazimika kuhairishwa kabla ya muda na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo Pandu Ameir Kificho, baada ya kuibuka kwa malumbano baina ya Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar Abubakar Khamis Bakari na Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka na kuchafua hali ya utulivu bungeni.

Mvutano huo uliibuka baada ya Mjumbe Abubakar Khamis Bakari kushitukia uwepo wa majina ya mapendekezo ya mabadiliko ya Mjumbe Ummy Mwalimu, Christopher Ole Sendeka na Peter Serukamba katika orodha ya Mwenyekiti, wakati orodha ya Kamati ya Rasimu ikiwa haina majina hayo.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS