Udhamini bado tatizo michuano ya netball EA
Chama cha netball Tanzania CHANETA kimesema kuwa maandalizi ya michuano ya klabu bingwa kwa nchi za Afrika Mashariki inayotarajiwa kuanza Machi 22 mwaka huu jijini Dar es salaam yamekamilika kwa asilimia 85.
Hii leo CHANETA ilikua katika uwanja wa taifa kukagua viwanja vitakavyotumika katika michuano hiyo, ambapo mwenyekiti wa CHANETA Bi. Anna Kibira, amesema kuwa licha ya kuwa mpaka sasa hawajapata udhamini wanataraji kuendesha michuano hiyo kama ilivyopangwa