Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano yasiyo na kikomo yalipangwa kufanywa leo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa madai ya kuporwa ushindi wa kiti cha Urais kwa Mgombea wao Edward Lowassa.