BASATA wapongeza Planet Bongo
Baraza la Sanaa Tanzania, (BASATA) kupitia afisa habari wao Aristideus Kwizera wamepongeza kipindi cha burudani cha Planet Bongo cha East Africa Radio kwa mchango wao katika kupiga muziki wa nyumbani na kuelimisha wasanii kuhusiana na sanaa yao.