Mgombea CHADEMA, aliyetoweka apatikana Hospitali
Mgombea ubunge jimbo la Mtwara mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joel Nanauka, aliyedaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha hatimaye ameonekana katika zahanati ya Bursa iliyopo manispaa ya Mtwara akipata matibabu.