CUF kuboresha kilimo na ujasiriamali Zanzibar
Mgombea urais wa Zanzibar kwa chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amewahakikishia wakulima serikali yake ikipata nafasi ya kuongoza itaweka mazingira mazuri wakulima na wajasiriamali kujiendeleza na kufaidika kimaslahi.