Jua Cali azidi kung'arisha mitaa
Rapa Jua Cali kutoka nchini Kenya amegusa nyoyo za wengi baada ya kutembelea kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu huko Kibera nchini Kenya, na kutoa msaada wa nguo, ikiwa ni namna yake ya kurejesha shukrani kwa jamii.